MABINGWA
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wamepunguzwa kasi baada
ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons Uwanja wa Sokoine
mjini Mbeya.Kwa
sare hiyo, Azam FC inatimiza pointi saba baada ya kucheza mechi tatu na
kushinda mbili- hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Mtibwa
Sugar yenye pointi sita.Mtibwa
Sugar watacheza kesho na Mgambo JKT ya Tanga Uwanja wa Manungu,
Turiani, Morogoro mchezo ambao wakishinda watapaa kileleni.Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wenyeji Polisi wametoka sare ya 1-1
na Kagera Sugar. Polisi walitangulia kupata bao kupitia kwa Nicholas
Kabipe dakika ya tano, kabla ya Rashid Mandawa kuisawazishia Kagera
dakika ya 88.Uwanja
wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wenyeji Ruvu Shooting wametoka sare
ya 0-0 na Mbeya City, wakati Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Coastal Union
wameshinda 2-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara. Mabao ya Coastal
yamefungwa na Joseph Mahundi dakika ya kwanza na Hussein Swedi dakika ya
26, wakati la Ndanda limefungwa na Nassor kapama dakika ya 57.Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, Simba imetoka 1-1 na Stand United ya
Shinyanga. Bao la Simba limefungwa na Shaaban Kisiga la Stand limefungwa
na Kheri Mohammed. Kikosi
cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael,
Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’, Gaudence Mwaikimba, Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche.Prisons;
Mohamed Yussuf, Salum Kimenya, Laurian Mpalile, Nurdin Chona, Lugano
Mwangama, Jumanne Elfadhil, Jeremiah Juma, Freddy Chudu, Ibrahim Hassan,
Amir Omar na Julius Kwanga.
MATOKEO YA LIGI LEO: Simba SC 1-1 Stand Utd, Coastal 2-1 Ndanda FC, Polisi 1-1 Kagera Sugar, Prisons 0-0 Azam FC, Ruvu Shoot 0-0 Mbeya City.
.Kesho;Yanga SC Vs JKT Ruvu, Mtibwa Sugar Vs Mgambo.
0 comments:
Post a Comment