Watu wengi barani Afrika wanatumia huduma ya Whats App kutumiana ujumbe mfupi
Janga la Ebola limewaua zaidi ya watu laki nne Afrika

BBC imezindua huduma mpya ya umma ya kiteknolojia inayotoa taarifa za afya kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kupitia kwa programu ya kijamii ya kutuma ujumbe mfupi kwenye internet ya 'WhatsApp.'

Programu hio inawalenga zaidi watumiaji wa Internet katika kanda ya Afrika Magharibi.
Huduma hio itawezesha wasomaji kupata taarifa kwa njia ya sauti, ujumbe mfupi na picha kuwasaidia kuepukana na maambukizi ya Ebola katika kanda nzima.


Taarifa zitakazopatiakana kwenye App hiyo zitakuwa angalau tatu kwa siku na huduma yenyewe itakuwa kwa lugha ya kiingereza na kifaransa.
Ili kupata taarifa kupitia kwa programu hiyo, tuma ujumbe mfupi...kupitia kwa WhatsApp kwa nambari +44 7702 348 651

WhatsApp ndio programu inayotumiwa sana kwa kutuma ujumbe mfupi barani Afrika na kwa kuitumia ina maana kuwa ujumbe huo utawafikia mamilioni ya watu barani Afrika kupitia kwa simu zao za mkononi.