Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama,
akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa
ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni
shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa
unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).
Shamrashamra
za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza
nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya
sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za
Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Mjadala
kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN
Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha
Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF),
ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha
mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa
vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa
Mataifa kwa ujumla wake.
Ijumaa
wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na
kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee,
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama
akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari
Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN
Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
0 comments:
Post a Comment