1.0 UTANGULIZIPamoja
na kutekeleza mpango wa kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau
kwa maana ya kufungua ofisi mikoani, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
umeanzisha mpango wa kupeleka huduma za Madaktari Bingwa mikoani.Mpango huu unawahusisha Madaktari Bingwa ambao ki-ukweli ni wachache kutoka katika hospitali zifuatazo:-
- Hospitali ya Taifa ya Muhimbili;
- Taasisi ya Mifupa MOI;
- Hospitali ya Bugando.
- Magonjwa ya Moyo
- Magonjwa ya Wanawake
- Magonjwa ya Watoto
- Upasuaji na
- Mabingwa wa Dawa za Usingizi.
- LENGO LA KUANZISHA MPANGO HUO:
- Kuwapeleka Madaktari Bingwa katika mikoa yenye uhaba mkubwa wa madaktari bingwa na kuwatumia wataalamu hao wachache kitaifa;
- Kuwapunguzia wananchi gharama za usafiri kufuata huduma za madaktari bingwa katika miji mikubwa;
- Kurahisisha utaratibu wa kumwona daktari bingwa ambao wanaonwa kwa ahadi maalum;
- Kuwapa fursa ya kujifunza na kuwajengea uwezo wa kiutendaji madaktari walioko kwenye hospitali za mikoa hiyo.
SN | MKOA | WAGONJWA WALIOONWA | WALIOFANYIWA OPERESHENI |
1 | Lindi | 258 | 6 |
2 | Kigoma | 754 | 37 |
3 | Katavi | 1276 | 37 |
4 | Rukwa | 1410 | 18 |
Jumla | 3,698 | 98 |
MKOA | TAREHE | MAHALI HUDUMA ZITAKAPOTOLEWA |
Mara | 3/11/2014-8/11/2014 | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara |
Tabora | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Manyara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) | |
Mtwara | Mipango ya maandalizi inaendelea (wanachi watajulishwa) |
- CHANGAMOTO ZA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI:
- Idadi ndogo ya Madaktari Bingwa ikilinganishwa na wananchi wanaohitaji huduma hizo.
- Uhaba wa vifaa tiba vya kisasa, kama vile vipimo katika hospitali za mikoa ya pembezoni na
- Uhaba wa vitendea kazi na madawa ili kufanikisha zoezi hili.
0 comments:
Post a Comment