Miss
Tanzania namba tatu, Jihan Dimachk. Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka
sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali
hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati
yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni
Jihan Dimachk.
Gumzo
mtaani kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti
Abbas Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la
Miss Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi,
maneno yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine
wakasema eti ana mtoto.
Kwenye fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss
Tanzania Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii
iliyofanyika kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo
Mikocheni, Dar.
Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey, nashukuru kuwafahamu, karibuni. Ijumaa: Tuanze na
matokeo ya kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe
ulistahili kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?
Jihan: Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa
nikiamini nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain
(haikuwa sawa ila siwezi kuelezea).
Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo? hebu fafanua kauli yako.
Jihan:
Sipendi kuwa muongeaji sana, naheshimu maamuzi ya majaji na Kamati ya
Miss Tanzania lakini ukweli uliopo moyoni mwangu ni kwamba nilijiamini
na ndiyo maana niliingia kwenye kinyang’anyiro nikijua ushindi ni haki
yangu.
Ijumaa: Wapo wanaosema ulikuwa na kila kigezo cha kuwa Miss Tanzania
2014 lakini umetoswa kutokana na rangi yako ukihisiwa wewe si Mtanzania,
unaliongeleaje hili? Jihan: Sipendi kabisa kusikia maneno hayo, mimi ni
Mtanzania, nimezaliwa Mwanza, mama yangu ni Msukuma na baba yangu
Mlebanon. Tangu naingia kwenye shindano hili waandaaji walinihoji,
wakafuatilia hilo na kutambua ni Mtanzania, ingekuwa tofauti sidhani
kama ningeruhusiwa kushiriki.
Ijumaa: Kwa mfano ikitokea Sitti akavuliwa taji kutokana na haya yanayozungumzwa, uko tayari uvishwe wewe?
Jihan: Siwezi kulijibu swali hilo kwani haijatokea. Endapo itatokea
na waandaaji wakanifuata kuniambia hivyo, hapo ndiyo nitakuwa na la
kuzungumza. Ijumaa:Unamuongeleaje Sitti Mtemvu? Jihan: Kwa sababu ndiye
aliyevishwa taji, naheshimu ushindi wake, namkubali kuwa ni mrembo na
siwezi kupingana na maamuzi yaliyotolewa.
Ijumaa: Umechukua nafasi ya tatu ambayo nayo si haba, una mipango
gani ya baadaye? Jihan: Nina mambo mengi ya kufanya. Nina ndoto za
kuwasaidia wanawake na watoto lakini pia nahisi nina jukumu la kusaidia
katika suala la elimu nchini, nitajipanga kufanikisha hayo. Ijumaa: Kwa
nini elimu?
Jihan: Nimekuwa nikikutana na watu wengi ambao elimu imekuwa kikwazo
kwenye maisha yao, nikawa nimejiapiza kuhakikisha nawasaidia kadiri
nitakavyoweza. Ijumaa: Asante sana Jihan, tunakutakia mafanikio katika
yale unayopanga kuyafanya.
Jihan: Nashukuru sana.
0 comments:
Post a Comment