Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Kimario.
Mwili
wa aliyekuwa Waziri mwandamizi kwenye serikali ya awamu ya kwanza na
pili Meja Jenerali (mstaafu) Muhiddin Mfaume Kimario umewasili leo
mchana kwa ndege ya shirika la Ethiopia kutoka nchini India alikokuwa
akipata matibabu tayari kwa mazishi siku ya Jumamosi mjini Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Mwili
wa Meja Jenerali Kimario uliwasili jana saa saba mchana kwenye uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JKNIA) na
kupokelewa na maafisa wa Jeshi, Serikali na wanafamilia.
Ijumaa
tarehe 10 Oktoba, 2014 Jenerali Kimario ataagwa kwa heshima za mwisho
kwenye kambi ya Jeshi Lugalo. Watu wote wanaotaka kushiriki kuaga mwili
wanakaribishwa. Tukio hilo la dakika 90 linatarajia kuanza saa 4 na
kukamilika saa 5:30asubuhi.
Baada
ya hapo mwili utapelekwa Msikiti wa Maamur ulioko Upanga kwa ajili ya
kuswaliwa wakati wa sala ya Ijumaa na baada ya kukamilika kwa sala hiyo
mwili utapelekwa uwanja wa JKNIA kwa ajili ya kwenda Moshi, Kilimanjaro
kwa ajili ya maziko siku ya Jumamosi.
Mazishi yake yatafanyika saa 10 jioni kwenye makaburi ya Moshi mjini baada ya kuswaliwa kwenye Msikiti wa Riadha.
Marehemu
Meja Jenerali Kimario atakumbukwa kama moja ya Maafisa wa kwanza
walioanzisha JWTZ, Kamanda wa vita aliyefanikisha kung’olewa kwa nduli
Iddi Amin, mwanasiasa shupavu aliyeshika nyadhifa mbalimbali kama Waziri
wa Ulinzi na Mambo ya Ndani pamoja na ukuu wa Mkoa kwa mikoa ya Mwanza
na Dar-es-salaam na Mkurugenzi wa CDA.
0 comments:
Post a Comment