Mahakama
ya Afrika Mashariki (EACJ), imeziagiza pande zinazohusika kwenye rufaa
ya kupinga hukumu ya kuzuia ujenzi wa barabara ya lami kupitia katika
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwasilisha hoja zao ifikapo Desemba 5,
mwaka huu.Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ya Tanzania, ambaye ndiye mrufani ametakiwa
kuwasilisha kwa maandishi hoja zake ifikapo Oktoba 22 na asasi isiyo ya
kiserikali ya Africa Network For Animal Welfare (ANAW) ya Nairobi, Kenya
ikitakiwa kujibu Novemba 21, mwaka huu.Jopo
la majaji watatu wa Kitengo cha Rufaa cha EACJ, Loboire Nkurunziza,
James Ogola na Edward Rutakangwa wanaosikiliza rufaa hiyo namba 3 ya
mwaka 2014, wamemwagiza mrufani kutoa majibu ya ziada ili Mahakama
ipange siku ya kusikiliza rufaa hiyo.Pande
zote zimekubaliana kushughulikia hoja zote nne za rufaa
zilizowasilishwa na Mwanasheria Mkuu, kupitia kwa Wakili wa Serikali,
Gabriel Malata.Katika
hoja zake, Serikali inadai Mahakama ya Awali ya EACJ ilikosea kisheria
kukubali kupokea, kusikiliza na kuamua shauri namba 9 la mwaka 2010
lililofunguliwa na ANAW kupinga wazo la ujenzi wa barabara hiyo yenye
urefu wa kilomita 239, ikidai itaathiri mazingira, uhai wa wanyama na
baionuai.Serikali
pia inakiomba Kitengo cha Rufaa kubatilisha hukumu ya mahakama ya
awali, kuamuru ilipwe fidia na gharama za kesi na amri nyingine kama
mahakama itakavyoamua.Katika
shauri la msingi, ANAW inayowakilishwa na wakili Kanchori Saitabau
ilitaja madhara kumi ya ujenzi wa barabara hiyo ikiwamo, kuongezeka kwa
shughuli za kibinadamu, kusumbua wanyamapori katika maeneo yao ya asili,
ongezeko la magari na uchafuzi wa hewa kutokana na moshi wa magari.Walidai
utekelezaji wa mradi huo unakiuka ibara za 5(3), 8(1), 111(2) na 114
(1) ya mkataba wa EAC unaelekeza wajibu kwa nchi za EAC kupanga na
kutekeleza sera na miradi yote iliyo chini ya mamlaka na wajibu wao kwa
kuzingatia uhifadhi wa mazingira
Friday, October 10, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment