JESHI
la Polisi Tanzania limefanikiwa kukamata mabomu manne ya kivita
yaliyofichwa katika eneo la mji wa Zanzibar na mtu ambaye jina lake
limehifadhiwa kutokana na sababu za kiuchunguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana makao makuu ya Polisi
Zanzibar, Kamishna wa Polisi Hamdan Omar Makame alisema kuwa Polisi
wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa uhalifu huo umewahi
kujitokeza siku za nyuma.
Kamishna Makame alisema kuwa mtu amewekwa chini ya ulinzi na
kuwaeleza polisi kuwa mabomu hayo yalikuwa matano lakini moja
lililipuliwa katika eneo la Darajani mjini Unguja.
Makame kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na ushirikiano baina
ya polisi na raia wema ambao wamekuwa wakichukizwa na vitendo vya
ulipuaji vinavyojitokeza katika nji huo.
Kamishna huyo hakuwa tayari kutaja jina la mtuhumiwa huyo wala eneo
waliokamata mabomu hayo kuhofia kuharibu uchunguzi na kutaka kuhakikisha
vitendo vya kihalifu vinatoweka na watuhumiwa wanachukuliwa hatua za
kisheria.
Februari 24, mwaka huu Watu wanne walijeruhiwa baada ya milipuko
minne inayoaminika kuwa ni mabomu kutokea katika maeneo matatu tofauti
Zanzibar.
Katika moja ya matukio hayo, watu wanne walijeruhiwa, mmoja akikatika
mguu, katika eneo la Unguja Ukuu, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
0 comments:
Post a Comment