Monday, October 20, 2014

Monday, October 20, 2014


A file photo taken on April 30, 2012 shows Zambia's President Michael Sata addressing the press at State House in Lusaka. PHOTO | AFP

Rais wa Zambia Michael Sata.

Rais wa Zambia Michael Sata, ambaye hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa sasa,ameondoka nchini humo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kiafya,taarifa kutoka ofisi ya rais imeeleza jumatatu.
Msaidizi wa rais Sata anayehusika na masuala ya habari Bw. George Chellah alisema kiongozi huyo mwenye miaka 77 aliondoka nchini Zambia jumapili lakini hakuweka wazi safari yake imeelekea wapi, au kueleza ikiwa ameenda kutibiwa.

"Mheshimiwa Michael Chilufya Sata, rais wa Zambia, ameondoka nchini usiku wa jana kwenda nje ya nchi ajili yakufanya uchunguzi wa kiafya.Mke wa rais Christine Kaseba, baadhi ya wanafamilia na waanishi wake wa habari wamemsindikiza kiongozi wa nchi," taarifa ya ikulu ilieleza.

Kumekuwa na uvumi kuwa Sata ni mgonjwa sana huku pia akishindwa kuonekana hadharani tangu aliporejea nchini Zambia mwezi uliopita kutoka Marekani kwenye mkutano mkuu wa umoja wa mataifa, ambako alitarajiwa kuhutubia lakini akashindwa.

Rais Sata alionekana hadharani Septemba 19 na kulieleza bunge: "Bado niko hai."

Mbali na kugua kwake kuendelea kukanushwa, wachambuzi wanasema tayari kumekuwa na msuguano wa kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi.

Zambia itasherekea miaka 50ya uhuru wake siku ya ijumaa wiki hiina viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya nje wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo ambazo Bw Sata ataziongoza.

CHANZO: Daily Nation

0 comments: