Vijana katika biashara ya uuzaji samaki
i Vijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki.
WAKATI
siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa vijana watakao shiriki
Shindano la Mashujaa wa Kesho ukiwadia na dirisha la upokeaji fomu hizo
kutarajiwa kufungwa leo Oktoba 10, 2014 majira ya saa nane ambapo idadi
ya vijana waliorejesha fomu hizo imeendelea kupanda. Akizungumzia
zoezi hilo jana mchana, Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil
Tanzania, Erick Mchome aliwataka vijana waliochukua fomu zao kuzirejesha
mapema ili kujipatia fursa ya kushiriki katika shindano hilo ambale
linaweza kuwakwamua vijana kiuchumi.
Alisema bado kuna idadi kubwa ya fomu ambazo hazijarejeshwa na vijana waliochukua fomu hizo na kuwataka kufanya hivyo kabla ya muda wa zoezi hilo kufungwa hapo kesho.
“Vijana waliorejesha fomu mpaka leo (jana) ni takribani vijana 200.
Zoezi zima la urejeshaji fomu litafikia tamati siku ya Ijumaa Oktoba 10, 2014 kabla ya saa nane mchana na baadaye kufanyika mchujo wa kupata vijana 40 watakaoingia hatua ya pili kabla ya kutangazwa washindi watano ifikapo mwezi wa 12.
Naye Mhadhiri wa Chuo cha Stella Maris ambaye pia ni Mratibu wa shindano hilo kituo cha chuo hicho, Justin Lusasi aliwataka vijana kutokata tamaa katika ushiriki kwani kitendo cha kushiriki pekee katika shindano hilo na kuingia hatua ya pili ni faida kubwa kwao kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kuaanda mipango ya biashara.

0 comments:
Post a Comment