Meneja
wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akizungumza katika
mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii juu ya maandalizi ya
tamasha hilo.
Meneja
wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam hii juu ya maandalizi ya
tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamsha, Issam Ramadhan na Kulia ni
Afisa Habari wa Karibu Music Festival, Said Hashim.
Meneja
wa tamasha la Karibu Music Festival, Richard Lupia akifafanua jambo
katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam hii leo juu ya
maandalizi ya tamasha hilo. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha, Issam Ramadhan
Tamasha
kubwa la Karibu International Music Festival, linataraji kufanyika
nchini kwa mara ya kwanza katika Pwani ya viwanja vya Taasisi ya Sanaa
Bagamoyo (TASUBA).Waratibu
wa Tamasha hilo Karibu Cultural Promotions kupitia kwa Meneja wa Onesho
hilo, Richard Lupia, amesema litafanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba
7-9 Mwaka huu wa 2014.Lupia
amesema vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 kutoka kila kona ya
dunia wanaopiga muziki wa dansi,Reggae, Hip Hop, Taarab, Ngoma za
Asili, Bongofleva na Ghani wanataraji kushiriki.“Lengo
kuu la Tamasha, pamoja kukazia katika kurasimisha tasnia ya muziki kuwa
na umakini zaidi, lakini kingine ni kukuza uchumi wa eneo husika la
Bagamoyo ambalo ni la kihistoria, pamoja na kuhakikisha sanaa ya asili
ya mtanzania inapata kuonekana katika jukwaa la kimataifa,”alisema
Lupia.Tofauti
na matamasha mengine yaliyowahi kufanyika Tanzania Bara, hili litakuwa
likitumia ala kwa asilimia mia moja, wasanii wote watakaoshiriki,
watalazimika kutumia muziki wa ala kuimba na sio Playback.Ukiachana
na burudani, wasanii pia watapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuunadi
muziki wao duniani kwa njia mbali mbali ambako kutakuwa na warsha kutoka
kwa wataalamu mbali mbali toka pembe zote za dunia.Tamasha
litakuwa likiendeshwa mchana na usiku ambapo mchana sanaa za michoro,
mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha huku semina na
mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa tanzania katika hatua nyingine
za kimaendeleo zikiwa zinaendelea.Mpaka
sasa zaidi ya vikundi 100 vimeomba kushiriki tamasha kutoka pembe mbali
mbali za dunia, tuko katika kuvichuja na kuangalia ubora wao, na Mungu
akipenda, wiki ijayo tutakuja tena kuwaambia majina ya wasanii
watakaoshiriki tamasha hili linalotarajiwa kuwa kubwa kuliko yote Afrika
ya Mashariki.Lengo
la kuja hapa mbele yenu kwa leo lilikuwa ni kuwajulisha kuhusiana na
hili na kutoa rasmi ombi letu kwenu la kusambaza ujumbe kuhusiana na
fursa hii kwa wasanii wetu kujifunza kutoka kwa wenzetu, jinsi wenzetu
kutoka nchi zinazoendelea, wanavyofaidika na sanaa yao ili na sisi
tuweze kujikomboa.Tunatanguliza
shukrani zetu kwa kuhudhuria kwanza, lakini kingine tunaomba
ushirikiano, bado sisi ni wachanga, tujitahidi kuhakikisha kwamba muziki
wa Tanzania unafika katika kilele cha mafanikio.
0 comments:
Post a Comment