Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya
uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi
ya binaadamu.Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta
amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu
serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.Kenyatta
amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya
baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha
leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa
kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo
ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.Upande
wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa
mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.
0 comments:
Post a Comment