Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum
la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la
vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania akiwaeleza waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa
wazalendo na kulinda amani iliyopo hapa nchini kwa maslahi mapana ya
Taifa. Aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum
la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni Mwenyekiti wa wa Shirikisho la
vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania akitoa wito kwa Watanzania kusoma
na kuelewa Katiba inayopendekezwa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na
watu wachache kwa maslahi yao.
Watanzania wametakiwa kuendeleza amani na mashikamano uliopo kwa
maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa kuenzi misingi ya Amani na
Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na aliyekuwa MJumbe wa
Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa
shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.¬ Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu wachache hivyo ni lazima tuwaepuke wote wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopoalisema MpanjuAkifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja ya
midahalo iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa
na watu wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo
vinaweza kuleta madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama
walemavu,wanawake na wataoto.Akizungumzia Katiba inayopendekezwa Mpanju amesema ni vyema
Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na
baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka
kauli zinazoweza kuleta uchochezi katika jamii hasa katika kipindi hichi
ambapo baadhi ya watu wamekuwawakitumia mwavuli wa Kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanya vitendo vinavyoashiria
uvunjifu wa amani.Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika
kupinga vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani hapa
nchini kwa kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya Taifa na si
ya Kikundi Fulani cha watu.Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha kuhusika na vurugu
zilizotokea katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es salaam na kudai
hahusiki na tukio hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .
0 comments:
Post a Comment