WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia Benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoani Pwani na kupora fedha kisha kumuua askari mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafary Mohamed ameuthibitishia mtandao
huu kutokea kwa tukio hilo na kwamba kwa sasa yupo njiani kuelekea eneo
la tukio.
"Taarifa hizo nimezipata kuwa watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi
kuvamia Benki ya NMB, Mkuranga na kupora fedha ambazo kiasi chake bado
hakijafahamika kisha kumuua askari mmoja aliyekuwa nje ya uzio wa eneo
hilo la benki ambaye hakuwa kazini ila walinzi wote wa benki wapo salama
na silaha zao hazijachukiliwa. Kwa sasa nipo njiani kuelekea eneo la
tukio kupata taarifa zaidi." Alisema Kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment