Kwenye kilichosikika jana June 25 2015
toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma ilikuwepo pia ishu ya Mbunge Martha
Mlata kuanzisha mjadala kuhusu amri ya Mahakama kwamba Mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi Sugu akabidhiwe mtoto wake ambae amezaa na Faiza
Ally kutokana na Mbunge huyo kuonekana kutoridhwishwa na malezi ya mtoto
akiwa kwenye mikono ya mama yake.
Ombi
likapokelewa kwenye meza ya Naibu Spika leo June 26 2015
>>>”Nimepokea ombi maalum la kuwasilisha maombi binafsi kutoka
kwa Mbunge Joseph Mbilinyi kwa hiyo namruhusu” >>> Naibu Spika Job Ndugai.
“Asante
sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015,
Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora
mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge
huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote
wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo”
“Hakutaja
jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii
mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa
mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph
Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi
anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah
Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia“
“Watu
wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani
sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia
matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“
“Mimi ni
mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia
hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto
wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012,
katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi,
nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa
anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha
tuhuma nzito“
“Mwanamke
anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima,
picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha
kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa
amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata
ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge“
“Nilienda
Mahakama ya Mwanzo Manzese, niliwashilisha ushahidi kwamba mzazi
mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June
23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe
kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni
amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata
kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
“Mashauri
haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata…
Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na
Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni
mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba
mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa” >>> Mbunge Joseph Mbilinyi.
0 comments:
Post a Comment