Wednesday, April 15, 2015

Wednesday, April 15, 2015

 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.

Mikoa iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni pamoja na Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa. Wakati zoezi likianza mikoa katika hiyo mashine nyingine zitakuwa zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mingine ni Singida Tabora Geita na Kigoma.

Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit alisema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.



 Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.

Dr Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (software) na upande wa Vichapishio (printer) ambavyo sasa vimetengenezwa nchini Ufaransa umeboreshwa na ni rahisi kusafishwa.

Mafunzo yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na yamezingatia sana upande wa Vichapishio (printer), Visoma alama za vidole (Finger Print Scaner) na kamera kutambua macho mekundu. Ameongoza kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya baada ya cha zamani kuharibika vimerahisishwa.

Kuhusu uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwamba kwa sasa tatitzo la mashine ya kuchukua alama za vidole wamelifanikisha kwa asilimia mia. Kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa alogarithim mpya ambao utatambua kila aina ya kidole.

Hata hivyo Kamera zimewekewa mfumo mpya wa kutambua macho mekundu na kurekebisha rangi ya macho mekundu (Red eyes) Bila kukwamisha zoezi la uandikishaji.

Mtarajio ni kwamba zoezi lauandikishaji liwe limekamilika ndani ya kila siku 28 tokea kila mkoa unapopokea mashine hizi. Vilevile Dr Sisit ameishukuru serekali kwa kufanikisha upatikanaji wa Vifaa “serikali imejitahidi kuandaa upatikanaji wa mashine hizo, na usafirishaji kwa njia ya ndege kwenda nchi nzima. Kila halmashauri na mkoa utachukua angalau siku 28 kukamilisha mkoa utakapo pokea Vifaa” Dr Sisit amesema.

Mwisho amesema kwamba mashine nyingine 1,600 zitawasili wakati wowote na kwamba serikali imetoa Dola za Marekani milioni 72 (Sh. bilioni 133).

Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya Nec kuwa imekwishapokea mashine 2,098, huku ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa. Alisema vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo imeingia mkataba na Nec na inaviagiza China.

0 comments: