Wednesday, April 15, 2015

Wednesday, April 15, 2015


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi (katikati
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Coastal Union na
viongozi wa mkoa,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Coastal
Union,Steven Mguto,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

VIONGOZI wa Klabu ya Coastal Union wamewatakiwa kushikamana vilivyo ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao iliyosalia katika Michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Magalula Saidi wakati alipokutana na viongozi wa timu hiyo ofisini kwa lengo la kufahamiana.Ujumbe wa Coastal Union, uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Steven Mguto.

Alisema kuwa muda uliobakia kwenye mechi za Ligi kuu sio wa kuanza kufikiria ni kitu gani kimetokea bali ni kuweka mipango imara na madhubuti itakayowapa mafanikio ili waweze kujipanga msimu ujao kwa ligi nyingine.

Aidha aliwataka viongozi hao kujiepusha na migogoro, mifarakano iliyokuwa na tija kwani hali hiyo ikiruhusiwa itashindwa kuwapa maendeleo na kukwamisha mipango yao waliojiwekea.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto alimuhaidi Mkuu wa Mkoa huyo kuyafanyia kazi kwa asilimia kubwa maelekezo aliyoyatoa ili waweze kupata mafanikio.

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Coastal Union, Akida Machai alisema changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo watazifanyia kazi kwa umakini mkubwa ili ziweze kuleta ufanisi katika michezo iliyosalia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa soka akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la soka Nchini (TFF) Khalid Abdallah.

0 comments: