Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha miswada mitatu ndani ya saa tatu.
Mmoja kati ya miswada hiyo ikiwa ni kitanzi kwa waandishi wa habari ambapo mwandishi atakayeandika takwimu za kutoka katika chanzo sahihi cha Serikali na baadaye kugundulika amepotoshwa na chanzo hicho atahukumiwa miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni kumi.

Miswada ambayo imepitishwa ni ile ya wakala wa usimamizi wa maafa ya mwaka 2014,muswada wa sheria ya usimamizi wa kodi wa mwaka 2014 pamoja na ule wa sheria ya takwimu wa mwaka 2013 ambapo umesababisha majibizano kati ya,Mbunge wa Ubungo John Mnyika,Mbunge Viti Maalum Ester Bulaya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju kuhusiana na kuwepo kipengele kisichofaa.
Kipengele hicho ni kile kinachosema mwandishi wa habari atakayeandika takwimu za kutoka katika chanzo sahihi cha Serikali na baadaye kugundulika amepotoshwa na chanzo hicho atalazimika kuchukuliwa hatua za kisheria na Serikali ikiwemo kifungo cha miaka mitatu ama kulipa faini ya shilingi milioni kumi ambapo wabunge hao wamekipinga ilhali mwanasheria mkuu wa Serikali amesema kinafaa.
Maazimio ambayo yamepitishwa bungeni hapo ni la kuridhia mkataba wa msingi na kanuni za utumishi wa umma na utawala barani Afrika la mwaka 2011 na lile la kuridhia makubaliano ya msingi ya ushirikiano katika bonde la Mto Nile .
0 comments:
Post a Comment