Thursday, March 26, 2015

Thursday, March 26, 2015
                           

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Arusha wamesema  hatua ya baadhi ya wananchi wanaomtembelea na kumshawishi waziri mkuu wa zamani Mh.Edward  Lowassa kuchukua fomu ya kugombea urais ikiendelea kupata tafsiri tofauti itakisambaratisha chama  hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha Bw. Issack Joseph amesema  hatua ya  baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho kukiuka misingi na taratibu zilizopo katika kurekebisha mapungufu yanayotokea ni dalili za kutosha  kuashiria kuwepo kwa Madahara makubwa ndani ya chama hicho,kama hali hiyo ikiendelea.
Aidha kiongozi huyo amesema kauli zinazotolewa za kumshambulia Mh.Lowasa ambaye pia ni mbunge wa Monduli bila kutolewa kwa maelezo ya kutosha kuonyesha kosa lake,zimetafsiriwa kwa mitazamo tofauti na wanachama wakiwemo wa mkoa wa Arusha ambao tayari wameanza kugawanyika jambo ambalo sio zuri kwa chama.
Kwa upoande wake mwenyekiti wa vijana wa chama hicho mkoa wa Arusha Bw.Robson Mollel,amesema hatua ya kushambuliwa kwa Mh.Lowasa kwa kitendo cha kutembelewa na watu nyumbani kwake ni uonevu na ukiukwaji wa haki yake ya msingi,yeye kama kiongozi, ya kuwasikiliza wananchi.

0 comments: