Thursday, March 26, 2015

Thursday, March 26, 2015
                          

Mkuu wa Wilaya ya Momba Richard Mbeho ametoa wiki mbili kwa mkandarasi anayejenga mradi wa maji katika kijiji cha Chilulumo, tarafa ya Kamsamba wilayani Momba kukamilisha kazi hiyo mara moja na wananchi wapate maji ili kuondoa malalamiko ya wakazi wa kijiji hicho ambao wanakabiliwa na adha kubwa ya uhaba wa maji.



Mkuu wa Wilaya ya Momba Bwana Richard Mbeho ametembelea kijiji cha Chilulumo ambako wananchi wamelalamikia tatizo la uhaba wa maji kwenye kijiji chao, huku mradi wa maji unaojengwa kijijini hapo kwa ufadhili wa benki ya dunia ukisuasua. 
Baada ya malalamiko hayo, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba kutoa maelezo juu ya tatizo la maji kwenye wilaya hiyo.
Baada ya kupokea maelezo hayo ndipoWkuu wa Wilaya akaagiza kukamilishwa kwa mradi huo wa maji haraka, huku akimtaka mkandarasi kumpelekea taarifa ya wananchi kuanza kutumia maji ndani ya kipindi cha wiki mbili.
Agizo hilo likamfanya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Momba, Bernard Sichilongwa kuwataka wakuu wa idara kuanza utekelezaji mara moja ili baada ya wiki mbili wananchi waanze kutumia maji yatokanayo na mradi huo.

0 comments: