Wednesday, February 4, 2015

Wednesday, February 04, 2015
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande



Mahakama Tanzania imesema imeweka mkakati wa kuwa na Mahakama ya Rufani kila mkoa pamoja na Mahakama Kuu kwa mikoa 12 iliyobakia kuhikikisha kuwa huduma zake zinapatikana popote nchini.
Hayo yalisemwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akifunga maonyesho ya Wiki ya Sheria jijini Dar es Salaam jana.
"Tayari tumeweka mkakati wa kuweka Mahakama ya Rufani nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kupata haki kwa wakati,” alisema Jaji Mkuu.
Alisema watu wengi wanapopata matatizo yanayohitaji msaada wa kisheria, hawajui mahali pa kwenda lakini baada ya maonyesho hayo, wengi wamejifunza namna ya kupata haki zao.
“Kwa mara ya kwanza Mahakama imeandaa maonyesho haya hapa jijini Dar es Salaam, lakini tunatarajia mwakani tutafanya mikoa yote ili wateja wetu wafikiwe na huduma zetu,” alisema Jaji Chande.
Aidha, alisema hali ya majaji kwa sasa inaridhisha kwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni 16 na Mahakama Kuu 80 na kwamba wamejipanga kumaliza mashauri yote ya zamani.

0 comments: