Wednesday, March 18, 2015

Wednesday, March 18, 2015
                             

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya basi la FM safari lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na fuso iliyokuwa imesheheni nyanya katika eneo la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lingine na hivyo kugongana uso kwa uso ambapo wametupia lawama baadhi ya abiria kuwachochea madereva kuendesha kwa kasi na kushauri vyombo vya usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva wazembe wanaosababisha vifo visivyo vya lazima.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amewataja walio fariki katika tukio hilo kuwa ni Seth Mapunda ambaye ni dereva wa fuso na mwanamke mmoja ambaye hajafahamika majina yake na jeshi la polisi linamshikilia dereva wa basi kwa kusababisha ajali hiyo. 

0 comments: