Monday, March 16, 2015

Monday, March 16, 2015
Rais wa Urusi amebeza uvumi na hisia zilizokuwa zikienezwa kuhusu afya yake baada ya kuonekana hadharani hivi leo kwa mara ya kwanza toka machi 5.

"Maisha hayawezi kupendeza bila kusemwa", alimwambia rais wa Kyrgystan Almazbek Atambayev kwenye mazungumzo yao mjini St Petersburg.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 62 alionekana mtulivu na alikuwa akitabasamu mbele ya kamera mbele ya kamera za runinga.
Kutoonekana kwake hadharani kulipelekea minong'ono na hisia kuwa huenda anaugua, amefariki,amepinduliwa, au kapata mtoto kwa mara nyingine tena.
Mapema jumatatu,Bw Putin aliamuru jeshi la majini la Urusi ukanda wa magharibi kukaa tayari kwenye bahari ya Aktiki.
Ndipo zaidi ya wanajeshi 45,000 ,wakiwa na ndege pamoja na meli za kivita walianza mazoezi makubwa ya kijeshi Kaskazini mwa Urusi.

Kyrgyzstan President Almazbek Atambayev (left) with Mr Putin



0 comments: