Sunday, April 5, 2015

Sunday, April 05, 2015

        Mtangazaji Charles Hillary (kulia) akiwa na mtangazaji mwanzake             wa BBC wakati akiagwa rasmi kituoni hapo, jijini London.

  Mmoja kati ya wafanya kazi wenzake akionesha jezi iliyoandikwa jina la Nkwanga.

        Charles Hillary  na mtangazaji wa BBC Zuhura Yunus katika picha.

                    Charles Hillary baada ya kuvaa jezi hiyo.

Aliyekuwa Mtangazaji wa BBC Charles Hillary ameaga rasmi jana kwenye kituo hicho na hivi punde atarudi nchini Tanzania kuendelea na kazi yake  ya  utangazaji katika kituo cha Television cha Azam TV.
Katika tasnia ya habari, Charles Hillary ni mtangazaji mzoefu ambaye amefanya kazi ya utangazaji kwenye vituo mbali mbali vya redio na televisheni ndani na nje ya nchi. Alianza utangazaji mwaka 1980 hadi mwaka 1993 Radio Tanzania Dar es Salaam kabla ya kuhamia Radio One Stereo mwaka 1994,ikiwa ni radio ya kwanza binafsi nchini Tanzania.
Mwaka 2003 aliacha kazi Radio One na kujiunga na Radio DW Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ambapo akianzia kazi mjini Koln na baadae kuhamia Bonn hadi mwaka 2006ambapo alilazimika kukatiza mkataba wake baada ya kupata ajira Idhaa ya Kiswahili ya BBC London,aliyojiunga nayo tarehe Aprili 14, 2006.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam. Mhariri wa BBC Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary. Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media,Tido Muhando alithibitisha Hillary kujiunga na Azam Media atakaporejea hapa nchini.
Jana Charles Hilary ameaga rasmi katika kituo cha utangazaji cha BBC na kuahidi kulitumikia taifa lake tena akiwa Azam TV.

0 comments: