Sunday, April 5, 2015

Sunday, April 05, 2015



Basi la klabu ya Fenerbahce lilifyatuliwa risasi na wapiganaji baada ya klabu hiyo ya Uturuki kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi klabu ya Rizespor.

Dereva wa basi hilo alipelekwa hospitalini lakini hakuna mchezaji aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hilo ambalo lilitokea wakati walipokuwa wakielekea katika uwanja wa ndege wa Trabzon.
Waziri Mkuu wa taifa hilo Ahmet Davutoglu amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
Shrikisho la soka nchini Uturuki limeshutumu shambulio hilo huku Katibu Mkuu wa klabu hiyo Mahmut Uslu akisema kuwa kitendo hicho ni cha makosa.
''Tulikuja hapa kucheza soka'', alisema Uslu ambaye alikuwa katika basi hilo wakati wa shambulio hilo.

0 comments: