Saturday, April 11, 2015

Saturday, April 11, 2015
Yusuph Mwenda's photo.

"Nimepokea heshima hii toka kwa mheshimiwa rais, kwa unyenyekevu mkubwa. Hii ni heshima na kazi kubwa wanayostahili kupewa waheshimiwa madiwani wa manispaa ya Kinondoni,Mkurugenzi na watendaji wote wa Manispaa, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa  Wilaya pamoja na wakazi wote wa Kinondoni kwa mchango wenu mkubwa kwa maendeleo ya Kinondoni.


Najua bado tunachangamoto nyingi, lakini kama tulivyoweza hapa tulipofika,kwa pamoja tutaweza kuifanya Kinondoni iwe na Maendeleo endelevu na sehemu bora zaidi ya kuishi Tanzania.

Mungu Ibariki Kinondoni"

Hii ndio kauli aliyoitoa mstahiki meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda, baada ya kukabidhiwa tuzo hapo jana.

0 comments: