Saturday, April 11, 2015

Saturday, April 11, 2015



                                        Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Bw. John Mnyika

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka watanzania kutambua, dawa ya migomo na migogoro kwenye sekta mbalimbali inayoendelea nchini ni kuiondoa CCM madarakani kupitia umoja wa katiba wa wananchi (UKAWA) kwenye uchanguzi mkuu ujao, kwa kuwa chama tawala kimeshindwa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi.



Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw.John Mnyika kwenye mkutano wa uchanguzi wa viongozi wa kanda ya kusini wa chama hicho uliofanyika mkoani Mtwara, na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chadema toka mikoa ya Mtwara na Lindi.

Uchaguzi huo umekuja katika kutekeleza sera ya majimbo kwa mujibu wa katiba mpya ya chama hicho ambapo ulichagua mwenyekiti wa kanda, makamu mwenyekiti, mratibu wa kanda, afisa wa kanda na kamati 6 za utendaji za kanda hiyo ya kusini katika kuimarisha chama na kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao.
Naibu katibu mkuu huyo wa Chadema John Mnyika amesema, taifa linapita kwenye migogoro na migomo inayoathiri uchumi na ustawi wa wananchi, na hivyo dawa ya kumaliza migomo na migogoro hiyo ni kuiondoa CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao huko akidai UKAWA ipo imara kutekeleza matarajio ya wananchi katika kushinda uchaguzi mkuu ujao.
Aidha baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa uchaguzi wamewataka wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura wakati utakapowadia, ili kufanikisha malengo ya Chadema na Ukawa kushinda kwenye uchaguzi mkuu ujao.  

0 comments: