Friday, April 10, 2015

Friday, April 10, 2015

Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.

Mgomo huo umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.

Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kuzungumzia suala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani  wamedai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.

Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.

Kwa picha hii waweza jiuliza, kwani daladala ndio huwa chanzo cha foleni?

Ilibidi tu watu wajivunie miguu yao kwa kuanza safari, hapo ni Ubungo
Wadau wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar wakiendelea na mijadala.
Hili lori lilizuiwa na watu wanaoaminika kuwa wasafiri waliokwama, wakimtaka dereva awashushe abiria aliokuwa amewapakia kama anataka kuendelea na safari.

0 comments: