Thursday, April 16, 2015

Thursday, April 16, 2015
Manuwari ya kivita ya Ujerumani wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Meli ya Uingereza ya SS City of Cairo ilizamishwa na manuwari ya Kijerumani wakati ikiwa imepakia tani 100 za sarafu kupeleka mjini London.

Timu inayoongozwa na uingereza  imeweka rekodi ya uzamiaji na uokozi kwenye vina virefu vya maji ya bahari katika historia baada ya kuibua sarafu zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 65 kutoka kwenye mabaki ya meli ya kivita ya Uingereza iliyozamishwa mwaka 1942. 


Timu hiyo imeibua sarafu kutoka kwenye iliyokuwa meli ya kiingereza ya  SS City of Cairo, ambayo ilizamishwa na manuwari ya Kijerumani Novemba 1942, ikitokea Bombay kuelekea Uingereza. Meli ilikuwa imebeba tani 100 ya sarafu za fedha, zilizokuwa mali ya Hazina ya Uingereza na zilikuwa zimeitishwa London kusaidia kufadhili hatua za kivita.

Meli hiyo ilizama mita 5,150 baada yakupigwa kombora na manuwari ya kivita Kijerumani maili 480 kusini mwa mji wa St Helena. Awali ilikuwa ikiaminika kuwa meli hiyo ilipotea mpaka mwaka 2011, ambapo wataalamu wa uvumbuzi wa maji ya bahari walipoanza kuitafuta baada ya kuingia mkataba na serikali ya Uingereza.

Kiongozi wa wagunduzi hao, Briton John Kingsford, alifanya ugunduzi huo baada ya kuona kitu kisichokuwa cha kawaida kilichotuama juu ya kilima. “Meli hiyo ilivunjika na kugawanyika vipande viwili  kabla ya kufunikwa na tope la kwenye sakafu ya bahari"

Sarafu hizo zilizokuwa zimetengenezwa kwa madini ya fedha zimeyeyushwa na kuuzwa kwa kiwango ambacho hakijawekwa bayana na mapato yake yamegawanywa kwa ya serikali ya Uingereza na wagunduzi hao.

Kabla ya kuzamishwa meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 311, japo wote walinusurika na shambulizi hilo lakini ni watu sita tu ndio waliofanikiwa kutoka hai baharini majuma kadhaa baadae. Manuwari ya Kijerumani iliyopiga kombora la kwanza na baadae kusubiri dakika kumi kabla ya kupiga tena kombora la pili, hali ambayo iliwapa nafasi abiria waliokuwa kwenye meli hiyo kutorokea kwenye boti za uokozi.

Karl-Freidrich Merten, aliyekuwa nahodha wa meli ya kivita ya Kijerumani aliwaongoza kuelekea kwenye kisiwa kilichokuwa karibu kisha akawaambia: “Usiku mwema. Poleni kwa kuwazamisha.”

Hapo ilikuwa ni wiki tatu kabla ya boti za uokozi walizopanda abiria hao kupatikana na kubainika kuwa abiria 104 kati ya 305 walikuwa wamekwisha fariki.

Baada ya kumaliza zoezi hilo, wagunduzi waliacha mnara kwa kumbukumbu ya watu waliofariki kwenye mkasa huo. Juu ya mnara huo yalisomeka maneno: "Tumekuja hapa kwa heshima"

0 comments: