Tuesday, May 26, 2015

Tuesday, May 26, 2015

Mamlaka nchini India zimebaini kuwa watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wamesajili kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48 katika kipimo cha Celsius, katika maeneo mengi nchini humo.

Vifo vingi zaidi vimeripotiwa kwenye ukanda wa kusini miji ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha, tangu jumamosi wimbi hilo la joto lilipoanza.

Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh, umelisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku mji mkuu wa India ,New Delhi ukistahimili kiwango cha nyuzijoto 44C .

Serikali nchini humo imeanza kampeni ya kuhamasisha wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri kunywa waji mengi.

Viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.

Vifo vingi vimerekodiwa katika jimbo la Andhra Pradesh, ambapo jumla ya watu 246 wamethibitishwa kupoteza maisha kuanzia juma lililopita.

"Asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.

Kwingineko, chama cha waandishi wa habari kimesema kuwa watu 186 wamefariki katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.

Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.

Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata, baada ya madereva wenzao wawili kufariki awali.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.

0 comments: