Tuesday, May 26, 2015

Tuesday, May 26, 2015
 


                                 Aliyekuwa kocha wa Real Madrid,Carlo Ancelotti.
 

Hatimaye miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wao Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.

Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya.

Pamoja na mafanikio aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa na wachezaji wazuri na wanaolipwa mishahara minono.

Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya huku klabu ya Barcelona, ambao ni wapinzani wao wakubwa, wakinyakuwa taji la ligi kuu ya Hispania na kutinga fainali ya klabu bingwa Ulaya.

Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahisi kuachana na kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.

0 comments: