Monday, June 22, 2015

Monday, June 22, 2015

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mh. Bernard Membe (kulia) akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali wakati wa kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri kwenye ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa  baba wa marehemu, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butiama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia)akiwa na Mama Maria Nyerere  katika shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri (wa tatu kulia), Butiama mkoani Mara Juni 21.2015.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipokwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butiama.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. John Guido Nyerere aliyefariki Mei 9 mwaka huu.

0 comments: