Mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein hivi leo ameendelea kampeni zake visiwani Pemba ambapo ameahidi kuboresha usafiri wa baharini kwa kununua meli kubwa na kuwaunganisha wazanzibari wote katika nyanja mbalimbali hasa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Katika mkutano alioufanya nyumbani kwao Chokocho kisiwani Pemba, Dkt. Shein amesema meli hiyo ambayo itakuwa ya mizigo na abiria ni sehemu ya ilani ya uchaguzi inayolenga kuunganisha na kuinua uchumi, kuboresha afya na kilimo cha karafuu pamoja na mpunga na kuwaondolea wananchi kero na umaskini.
Katika mkutano huo, mmoja wa makada wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Omary Yusufu Mzee alipopanda jukwaani alieleza hofu ya chama chake kwa kile alichokiita kubaini mbinu za kuibiwa kura na hivyo kutahadharisha kuwachukulia hatua watendaji na wasimamizi wa uchaguzi kwa yeyote atakayehusika na kuwa nyuma ya mpango huo.
0 comments:
Post a Comment