Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mwmvuli wa vyama vinavyounda UKAWA Mh. Edwad Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa kipaumbele cha elimu pia kinatolewa kwa wakulima wafugaji na makundi mengine hatua itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa tija na kupokea teknolojia za kisasa.
Akizungumza na umati mkubwa wa wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu,ambao asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji,Mh lowasa amesema pamoja na azima yake ya kutoa elimu bure mashuleni pia itakuwa bora yenye mafanikio yanayoonekaana kwa vitendo kwa wananchi wengine.
Aidha Mh Lowassa amesema elimu ikitumika viziri na watu wote wakaelimika umaskini utapungua na pia unyanyasaji wa watu wa kipato cha chini utapungua.
Waziri Mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredrik Sumaye amesema asilimia kubwa ya matatizo yanayowakabili wakulima na wafugaji wakiwemo wa mkoa wa Simiyu ni matokeo ya kukosa misingi imara inayo changiwa na mfumo mbaya wa elimu na ndio maana UKAWA imeweka msukumi mkubwa katika elimu kama wananchi wakiichagua kuingia madarakani.
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi Bw Godwin Samba amewaomba wananchi wa Bariadi wamchague yeye na viongozi wengine wa UKAWA ili wamalize matatizo sugu yanayo wakabili wakulima na wafugaji kwa muda mrefu sasa.
Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Simiyu anaendelea kunadi sera ya mabadiliko katika mkoa wa Kagera.
0 comments:
Post a Comment