Tuesday, July 14, 2015

Tuesday, July 14, 2015
IMG_20150714_094525
Maisha Basement zamani ilikuwa ikiitwa New Maisha Club kwa sasa imehamia Makumbusho Kijitonyama kwenye jengo jipya la LAPF Towers. Club hii ni mpya na ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukua watu mia saba (700) kwa wakati mmoja, yenye vifaa vya kisasa na dance floor ya kisasa yenye uwezo wa kurusha matukio live kama video na mechi za mpira.
Uzinduzi wa Maisha Basement utafanyika kwa siku 3 tofauti, uzinduzi wa kwanza utakuwa Jumatano ya tarehe 15/07/15 ambapo tutazindua na watu maarufu mbalimbali, na uzinduzi wa pili utakuwa Alhamisi ya 16/07/15 na siku hii tutawaalika watu mbalimbali kutoka katika makampuni (Corporate People).
Na uzinduzi rasmi wa MAISHA BASEMENT utakuwa siku ya eid mosi, ambapo tutakuwa na burudani mbalimbali, na mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda. Siku hii kiingilio kitakuwa shilingi elfu kumi tu. Awali, burudani zilikuwa zinaanza Jumatano mpaka Jumapili, lakini hapa Maisha Basement burudani zitaanza Jumatatu mpaka Jumatatu.
IMG_20150714_095034IMG_20150714_095103IMG_20150714_095432IMG_20150714_100546

0 comments: