Monday, July 13, 2015

Monday, July 13, 2015



Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa Matteo Darmian kutoka Torino. Matteo amesaini mkataba wa miaka minne, ambao una kipengele cha kuongeza tena mwaka mmoja hapo baadae.

Darmian, 25, amecheza michezo 146 ya kwenye ligi, na kufunga magoli 5 tangu alipojiunga na klabu ya Torino mwaka 2011. 

Mlinzi huyo ameichezea timu ya taifa ya Italia mara 13, na alikuwa katika kikosi cha Italia kwenye kombe la dunia mwaka jana Brazil.

Matteo Darmian alisema: “Ni ndoto iliyotimia kujiunga na Manchester United.Nimefurahia muda nilioutumia nikiwa Torino na ningependa kuishukuru klabu na mashabiki kwa yote waliyonitendea. Naamini wataelewa kwamba wakati fursa ya kujiunga na klabu kubwa duniani inapokuja basi hilo ni jambo ninalopaswa kulikubali".



0 comments: