Hatimaye Liverpool wamekubaliana na Manchester City kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 49 wa winga Raheem Sterling.
Uhamisho wa winga huyo mwenye miaka 20, sasa utategemea makubaliano ya mkataba na vipimo vya afya atakavyoanyiwa mchezaji hivi karibuni.
Sterling aliomba kuondoka Anfield, huku dau la City likikataliwa mara mbili mwezi Juni.
Ikiwa dili hilo litakamilika basi Streling atakuwa mchezaji ghali zaidi kutoka England
Mkataba wake kwenye klabu ya Liverpool unaisha mwaka 2017, lakini aligoma kuuongeza baada ya kukataa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki.
Siku ya Jumamosi, Sterling alitajwa katika kikosi cha wachezaji 30 wa Liverpool wanaokwenda Thailand, Australia na Malaysia, lakini baadaye jina lake liliondolewa baada ya mchezaji huyo kutoonyesha utayari wa kuungana na kikosi hicho kwenye safari baada ya 'kujisingizia' ugonjwa.
0 comments:
Post a Comment