Monday, August 24, 2015

Monday, August 24, 2015
Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chadema,
Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea akionyesha kadi za kupigia kura jana zilizodaiwa kukamatwa hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ambaye pia ni  mgombea wa Kawe, Halima Mdee.
Wagombea ubunge wa majimbo ya Kawe na Ubungo kwa tiketi ya Chadema wamedai kubaini kadi za kupigia kura 100 ambazo hazina taarifa
Akizungumza waandishi wa habari,Bw. Kubenea alisema, "hapa tunazo 100, lakini tume imeandaa kati ya kadi 2,000 hadi 3,000 ambazo zitatumika kuwaandikisha wapiga kura wengine kwa lengo la kuisaidia CCM."
Mgombea wa Kawe, Halima Mdee alisema uhakiki wa daftari la mpigakura unapaswa kufanyika kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura na sio ofisi za kata. Alisema kata yenye watu 70,000 haiwezi kuhakiki wananchi wote ndani ya muda wa siku 4 zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi
Mdee aliendelea kusema kuwa wamepata taarifa kuwa wakimbizi 70,000 wameandikishwa kwa siri kwenye daftari hilo mkoani Kigoma.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC Bw. Kailima Kombwey alisema hafahamu kuhusu kadi na kushauri suala hilo lipelekwe polisi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

0 comments: