Monday, August 24, 2015

Monday, August 24, 2015
Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita - ICC wanaangalia uwezekano wa kumpunguzia kifungo kiongozi wa zamani wa wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Thomas Lubanga (pichani)anayetumikia kifungo cha miaka 14 jela.

Lubanga alipatikana na hatia kwa makosa ya kusajili askari watoto katika jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2002 na 2003 na amekuwa gerezani mjini Hague kwa miaka minane sasa.

Kwa mujibu wa taratibu za mahakama hiyo ya ICC, Thomas Lubanga alikamilisha robo tatu ya kifungo chake jela mwezi uliopita hatua ambayo majaji hao wanasema inaweza ikatoa fursa kwao kumpunguzia adhabu kwa kumuachilia mapema zaidi.

Thomas Lubanga anatajwa kuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya ICC ambapo sasa anadai anataka kurejea nyumbani ili kusomea chanzo cha mapigano ya kikabila.

0 comments: