RAIS Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki alikutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Mafuta ya Total, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo katika Afrika Mashariki, Javier Rielo (pichani).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, ujumbe huo wa Total kutoka makao makuu ya Kampuni hiyo katika Afrika Mashariki yaliyoko Kampala, Uganda, umemweleza Rais Kikwete kuhusu mipango ya ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Kampuni hiyo imemweleza Rais Kikwete kuwa ingependa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Ziwa Albert, ambako Uganda inachimba kuzalisha mafuta, hadi kwenye Bahari ya Hindi kwa ajili ya kuyasafirisha kwenda kwenye masoko ya nje.
Rais Kikwete ameishukuru kampuni hiyo kwa mpango wake huo wa ujenzi wa bomba hilo la kusafirisha mafuta lenye urefu wa kilomita 1,400.
0 comments:
Post a Comment