Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima (kulia) na Miss Kenya, Idah Nguma (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na mdau wa Hospitali ya CCBRT iliyopo Msasani jiini Dar es Salaam, baada ya kutembelea hospitali hiyo
MISS Kenya 2015 Idah Nguma ametembelea nchini Tanzania kwa ajili ya kutembelea Hospitali ya CCBRT kuwafariji wagonjwa pamoja na kuona huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.
Katika ziara ya kutembelea hospitali hiyo Nguma aliongoza na mwenyeji wake Redds Miss Tanzania 2015, Lilian Kamazima na mmoja wa maofisa wa kamati ya kuratibu Miss Tanzania.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Dar es Salaam leo asubuhi ,Nguma alisema amefurahi kuja nchini hapa kwa mara ya kwanza huku lengo lake likiwa ni kuangalia mradi wa Smile Train ambao upo Switzerland.
Nguma alisema mradi huo ni wakusaidia wanawake wenye festula pamoja na watu wenye matatizo ya mdomo wazi.
"Mimi ni Balozi katika shirika hilo na nimekuja kuangalia huduma kwa wagonjwa wa Fistula na Midomo wazi (sungura)" alisema Nguma.
Nguma alisema amefurahishwa na huduma inayotolewa na wahudumu waliopo katika hospitali hiyo pia atakapofika katika ziara yake ya kwa nchi ya Uganda atawaelimisha jamii na wananchi wa Uganda kwa huduma bora wanyopata watu wenye matatizo hayo.
Pia hata Miss wa Tanzania Lilian Kamazima amesema kuwa wamemkaribisha kwa furaha Miss wa Kenya hiyo yote ni kudumisha amani na upendo katika nchi hizi mbili.
Alisema ziara yake ya kuwaona wagonjwa ni moja ya kuonyesha kuwajali wagonjwa na kudumisha upendo na kuwapatia faraja na kuowaongezea matumaini ya kuona kuwa na wao ni miongoni mwa watu katika jamii.
"Nimefurahishwa na huduma inayotolewa katika hospitali hiyo hasa baada ya kuona wagonjwa wanaendelewa vizuri""alisema.
0 comments:
Post a Comment