Saturday, August 22, 2015

Saturday, August 22, 2015

Watu wasiojulikana wamevamia na hatimaye kubomoa nyumba ya mgombea ubunge jimbo jipya la Nanyamba wilaya ya Mtwara vijijini kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF, Bw.Twahiri Saidi, usiku wa kuamkia leo, baada ya mgombea huyo kushindwa kurudisha fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku simu zake za mkononi zikiwa hazipatikani.

Wanachama na baadhi ya viongozi wa CUF wamezungumzia tukio hilo kwa masikitiko na kusema mazingira aliyotoweka mgombea huyo yanaonyesha wazi kuna mchezo mchafu umefanywa ili kutoa fursa kwa mgombea wa CCM Abdallah Chikota kupita bila kupingwa katika jimbo hilo.

Kwa upande mwingine Katibu wa Kata ya Milango Minne eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.

Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo na baada ya maneno hayo simu zake hazikuweza kupatikana mpaka muda huu.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa nanyamba, Bw. Oscar Ng’itu akiongozana na mkuu wa kituo cha polisi Nanyamba wamembelea nyumba iliyobomolewa na kutoa agizo kwa wananchi kuwataja watu waliyohusika na tukio hilo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo wake.

0 comments: