Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es salaam, uliohudhuriwa pia na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),Sumaye amesema lengo lake ni kuimarisha upinzani ili kuleta mabadiliko yanayohitajiwa na wananchi nje ya CCM.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA VIDEO
Awali, Mh.Sumaye alitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusu taarifa zilizotolewa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwamba amejitoa CCM na kujiunga na ukawa,
Fredrick Sumaye,alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa kuanzia mwaka 1995 mpaka mwaka 2005.
0 comments:
Post a Comment