Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wameendeleza ubabe kwa Azam FC katika michezo ya ngao ya jamii baada ya leo kuibuka na ushindi wa penati 8-7 ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo mbele ya Azam FC katika mchezo ya ngao ya jamii.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jioni ya leo, ulikuwa wa kasi ya hali ya juu katika kipindi cha kwanza huku kila timu zikishambuliana kwa zamu, na kushuhudia umaridadi wa makipa Aishi Salum Manula na Ally Mustapha ambao walifanya kazi ya ziada kuokoa michomo ya hatari.
Katika kipindi cha pili, hasa baada ya kuingia kwa Haruna Niyonzima kuchukuwa nafasi ya Said Juma Makapu, mambo yakawa tofauti kwa Yanga kutawala zaidi mchezo na kuiweka katika wakati mgumu ngome ya Azam, ambao walitumia muda mwingi kutafuta mpira na kutengeneza mashambulizi machache lakini yaliyokuwa ya hatari zaidi ya yale ya wapinzani wao
Baada ya dakika 90 kumalizika, Azam ndio walianza upigaji wa mikwaju ya penati na wakapata goli la kwanza kutokana na mkwaju maridadi uliopigwa na mchezaji Kipre Tchetche kabla ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub kukosa.
Mpaka mwisho, Yanga waliibuka washindi baada ya kupata penati 8 dhidi ya 7 za Azam ambao walipoteza penati mbili kupitia wachezaji Pascal Wawa na Ame Ally Zungu.
0 comments:
Post a Comment