Thursday, August 20, 2015

Thursday, August 20, 2015

Rais Jakaya Kikwete ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhakisha inasimamia vyema upatikanaji wa haki kwa watu wote bila kujali hali zao, kwani kutofanya hivyo ni wazi kuwa nchi inaweza kugeuka kuwa uwanja wa dhuluma na mateso kwa raia ambao ni wanyonge.

Mh Kikwete ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuagana na watumisha wa Tume, na kuendelea kusema kwamba nchi isiyokuwa na utawala wa sheria ni sawa na watu wanaoishi katika msitu ambapo mwenye nguvu ndio anayeishi salama.
Aidha rais Kikwete ameonyesha kusikitishwa kwa namna ambavyo tatizo la migogoro ya ardhi linavyozidi kukua nchini na kusema kuwa rushwa ni moja ya sababu kubwa inayosababisha hali hiyo kuendelea na hivyo ni lazima hatua za dhati zichukuliwe.

Kwa upande wake mwenyekiti wa tume hiyo Mh Bahametom Nyanduga amesema katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchaguzi mkuu ni vyema kila mtu na hasa Jeshi la Polisi kuzingatia utawala wa sheria ili kuhakisha kuwa uvunjifu wa amani hautokei.

0 comments: