Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatoa hofu watanzania kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu imejiimarisha kimfumo wa kielektronic kuhakikisha matokeo yote yanayopatikana yanatangazwa ndani ya kipindi kifupi na ikiahadi kutangaza matokeo ya jumla ya kura za rais ndani ya siku tano.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasema katika kipindi hiki hakutakuwa na dosari zozote za kimfumo hasa taarifa za wagombea huku ikijinasibu kuwa kupitia mfumo wake mpya wa kupokea, kuhesabu na kujumlisha matokeo ambao uko kielektroniki hakutakuwa na ucheleweshaji wa kutangaza matokeo.
Mwenyekiti wa Tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva(pichani), ameviasa vyama vyote kufuata kanuni na sheria za uchaguzi katika kampeni kwani kushindwa kufanya hivyo nikuilazimisha Tume kuchukua hatua kali za kisheria.
0 comments:
Post a Comment