Thursday, September 3, 2015

Thursday, September 03, 2015
Watanzania hasa vijana wametakiwa kutafakari kwa kina mustakabali wa taifa letu,katika wakati huu wa uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi ambao hawatakuwa vibaraka wa mataifa mengine kwani Tanzania ina maliasili nyingi ikiwemo gesi na mafuta ambayo huenda mataifa hayo yakautumia uchaguzi huu kuwaweka madarakani vibaraka wao na kuifanya nchi kuwa mhanga wa maliasli zake kwa kushindwa kufikia malengo ya kuwaondolea umasikini watanzania.

Hayo yamesemwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli wakati akizungumza na viongozi wa ngazi za juu wa jumuia ya wazazi Tanzania ambapo kupitia kwao amewataka kuwaelimisha vijana juu ya kufanya mabadiliko ya pupa bila kujali athari za kesho kwa kuwa mjuto ni mjukuu.

Aidha Dr Magufuli ameendelea kusisitiza suala la kutunzwa kwa amani ya Tanzania na kwamba watanzania wasikubali kufarakanishwa kutokana na itikadi ya vyama vyao na kuwataka kumwamini kuwa ana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla kama china ilivyofanya badala ya kufanya mabadiliko ya jazba kama nchi za Libya.

Mwenyeikiti wa jumuia ya wazazi wa chama cha mapinduzi ndg. Abdala Bulembo amwakikishia mgombea huyo kuwa jumuia imejipanga kumsemea ili aendelee kuaminiwa na watanzania kwani kazi alizozifanya zinaeleweka na kuheshimiwa na watanania.

0 comments: