Thursday, September 3, 2015

Thursday, September 03, 2015
Mgombea urais kupitia mwamvuli unaounda UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akipata ridhaa ya wananchi na kuwa rais wa awamu ya tano ataunda tume ya kushughulikia na kutoa haki kwa wananchi wakiwemo wa mkoa Katavi walioathiriwa na operesheni tokomeza na wanaoendelea kukumbwa na umaskini kutokana na migogoro ya ardhi.

Akizungumza na maelefu ya wananchi kwenye maeneo mbalimbali mkoani Katavi Mh Lowassa amesema asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakiteseka kwa kutokana na viongozi wengi kutokuwa na uwezo wa maamuzi ama kutoa maamuzi yasiyo sahihi,suala ambalo serikali atakayoiunda haitalifumbia macho hata kidogo.

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuungana na viongozi wanaotoka CCM kuhamia UKAWA kutokana na viongozi wa CCM kukithiri kwa uonevu aliofanyiwa Mh Lowassa na viongozi wengine waliokuwa wanawania nafasi ya urais ambao walionekana hawafai.

Baadhi ya viongozi waliokiama Chama cha Mapinduzi akiwemo Hamisi Mgeja wamesema sera za UKAWA ni tofauti na zingine kwani zimelenga kuunda serikali ya wananchi na wala sio ya viongozi kama zinavyosema za vyama vingine.

Mgombea ubunge wa jimbo la Mpanda Mh Jonas Kalinde na baadhi ya wananchi wamesema mabadiliko chini ya UKAWA yanadhihirisha kwa vitendo jinsi wananchi walivyochoshwa na serikali ya CCM ambayo imekuwa ya maneneo yasiyo na utekelezaji.

0 comments: