Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es jana juu ya kufanyika kwa maonyesho ya
utalii yanayoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
======= ======= ==========
ONESHO
la kimataifa la utalii ‘Swahili International Tourism Expo’ (SITE)
linaloandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) linafunguliwa rasmi
kesho Jumatano katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na
litamalizika Jumamosi.
Tayari
maandalizi yote kuelekea ufunguzi wa onesho hilo yamekamilika na kwamba
watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vivutio adhimu
wa taifa hili.
Shirika
la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro
(NCAA) pamoja na Shirika la Ndege la Ethiopia ndio wadhamini wa onesho
hilo linalotarajiwa kushirikisha mataifa mbalimnali ulimwenguni.
Wadhamini
wengine ni pamoja na Zanzibar collection, Hoteli za Sea Cliff, Serena
hotel, Southern Sun,NewAfrica, Hyatt Regency,Protea, Serena hotel,
Bouganvillea Safari lodge, Acacia Farm lodge na Soroi Tented Camp
zimedhamini huduma ya malazi kwa wageni maalumu.
Pamoja
na washiriki wengine onesho hilo linatarajiwa kushirikisha wafanya
biashara wakubwa na watalii kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani pamoja
na wandishi wa habari wa kimataifa wanaokuja kwa ajili ya onesho hilo.
Wakati
Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa ikitoa udhamini wa
mabasi ya kubebea washiriki wakati wa onesho hilo, benki ya CRDB imetoa
udhamini wa fedha taslimu na inatarajiwa kuwa na banda ndani ya maonesho
hayo ya aina yake.
Usafiri wa ardhini utadhaminiwa
na makapuni Zara Tours, Naeda Safaris Ltd, Wildlife Expedition Safari,
huku Azam Marine wakijitokeza kudhamini usafiri wa baharini kutoka
Zanzibar. Mashirika ya ndege ya Rwandair, Precision Air na Uturuki
(Turkish airline) yatatoa tiketi za ndege kwa ajili ya kuwasafirisha
baadhi ya wageni wakati wa onesho hilo.
Makampuni mengine yaliyojitokeza ni yale yanayomiliki majarida. Haya ni Event, Dar Life na 7th Floor Media kutoka hapa nchini na Go Places kutoka Kenya, ambavyo wanatangaza onesho hili kupitia majarida yao.
Aidha
kampuni ya Montage imetoa udhamini wa kuwa mpambaji katika kumbi za
mikutano. Boogie woogie pia wametoa udhamini na watakuwa na mgahawa wao
wa chakula katika banda la utalii wa utamaduni ilhali wadhamini wengine
Black Tomato wao watakuwa na banda la kuuza kahawa ya Tanzania.
‘Swahili International Tourism Expo’ litakuwa likifanyika kila mwaka mnamo mwezi wa Oktoba na kuhudhuriwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment