BALOZI Mwanaidi Sinare Maajar ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Benki ya Afrika (BOA) na kuidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na benki hiyo, Balozi Maajar ambaye ni Mwanasheria aliyebobea anachukua nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Balozi Fulgence Kazaura, aliyefariki dunia mapema mwaka huu.
“Balozi Maajar ana uzoefu wa kutosha wa masuala mbalimbalimbali yanayohusu sekta za umma na binafsi,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa chini ya uenyekiti wake benki inatarajia kusonga mbele zaidi.
Mwenyekiti mpya wa Bodi alimaliza kutoa huduma yake ya kazi akiwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Balozi asiye mkazi Mexico(non-resident ambassador) mwaka 2013.
“Balozi Maajari ni miongoni mwa waasisi Partner of Maajar, Rwechungura, Nguluma & Makani, Advocates, (“MRN&M”) ambapo Februari 2006 MRN&M iliungana na kampuni nyingine ya Epitome Advocates na kuunda REX ATTORNEYS (“REX”) .
Kwa sasa Balazi Maajar ni mwenyekiti pia wa Kituo cha Ushikiano kati ya Tanzania na Msumbiji, Vodacom Tanzania and the International Consultant for the D Group.
Katika upande wa kijamii, Balozi Maajar ni Mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust (HMT), asasi iliyoanzishwa julai 2011 inayojishughulisha na kuboresha mazingira ya kusomea shuleni hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment